✨ Naibu Waziri Mkuu wa Urusi Dmitri Chernishenko alikutana na wajumbe kutoka Tanzania, katika Tamasha La Kimataifa la Vijana!
🪆 Dmitri Chernishenko alitembelea banda la "Urusi pamoja nawe", ambapo Naibu Mkuu wa “Rossotrudnichestvo”- Konstantin Kolpakov alitoa maelezo: "Matryoshka yetu" ina ofisi ya mradi, ambayo inatumika kama dirisha la kupokelea maoni kutoka kwa washiriki wa kigeni na pia wa Kirusi. Rossotrudnichestvo itasaidia katika utekelezaji wake kwa utaratibu wa ruzuku, ambao utazinduliwa mwaka 2027. Lakini Matryoshka pia ni dirisha la ushauri katika Majumba ya Urusi duniani kote".
📱☎️ Washiriki wa Tanzania katika Tamasha hilo waliwasiliana na Jumba la Urusi la Dar Es Salaam na kuelezea kuhusu mawazo yao.
📝 Hayo yatatekelezwa kama sehemu ya mpango wa "Kizazi Kipya" kwa ajili ya viongozi kutoka duniani kote, ambao watakuja Urusi ili kuongeza utaalam wao na pia kufahamu utamaduni wa Urusi.
🤝 D. Chernishenko alilishukuru Shirika kwa mradi huu wa Kitaifa wa "Vijana na Watoto".
Post #8725
114




